Kufanya kazi kwa pamoja ili kukaa salama mtandaoni

Kuweka mtandao ukiwa salama kwa kila mtu ni wajibu wa watu wote. Jifunze unachoweza kufanya ili kujilinda wewe na familia yako mtandaoni.

Kwa kila mtu

Jifunze kuhusu zana za usalama za Google zilizoundwa kukusaidia kudhibiti usalama na faragha ya data yako ya kibinafsi.

Pata maelezo zaidi

Kwa familia

Isaidie familia yako ijifunze mazoea mazuri ya kiusalama ukitumia zana kutoka Google na ushauri kutoka kwa washirika wetu wa usalama wa familia.

Pata maelezo zaidi

Zana za usalama

Sanidi zana rahisi za usalama na upate maelezo zaidi kuhusu kukaa salama kwenye Gmail, Chrome, YouTube, na bidhaa nyingine za Google.

Chrome

Vinjari wavuti kwa faragha

Unaweza kutumia Hali Fiche katika kivinjari cha Chrome kwenye kompyuta yako, kompyuta kibao, au simu ili kuvinjari wavuti kwa faragha. Katika Hali Fiche, kurasa unazotembelea na faili unazopakua hazirekodiwi katika historia ya kuvinjari au kupakua ya Chrome.

Pata maelezo zaidi

Bofya Menyu ya Chrome kwenye upau wa kivinjari wa vidhibiti → Bofya Dirisha Fiche Jipya.

Dirisha jipya litafunguka na ikoni ya chini kwa chini katika kona. Ili kuondoka, funga tu dirisha.

Android

Toa uwezo wa kufikia programu na michezo iliyoidhinishwa pekee

Je, unataka kushiriki kompyuta kibao yako pasipo kushiriki chochote kingine? Kwenye kompyuta vibao za Android zenye toleo la 4.3 na matoleo mengine mapya, unaweza kuunda wasifu wenye vizuizi ambao utadhibiti uwezo wa watumiaji wengine kufikia vipengele na maudhui kwenye kompyuta kibao yako.

Pata maelezo zaidi

Kama ni wewe unayemiliki kompyuta kibao, gusa Mipangilio → Watumiaji → Ongeza mtumiaji au wasifu.

Gusa Wasifu ulio na vizuizi → Wasifu mpya kisha uupe wasifu jina.

Tumia vitufe vya WASHA/ZIMA na mipangilio ili udhibiti ufikiaji kwa vipengele, mipangilio na programu.

Bonyeza kitufe cha kuwasha/kuzima ili urudi kwenye skrini ya kufunga, kisha gusa ikoni ya wasifu mpya.

Ikishawekwa, skrini ya Mwanzo huwa haina chochote. Gusa ikoni ya Programu Zote ili uanze kutumia wasifu mpya.

Angalia zana zingine za usalama