Njia rahisi na salama zaidi ya kuingia katika Akaunti yako ya Google
Funguo za siri ni njia salama na rahisi zaidi ambayo hutumika badala la manenosiri. Hukuruhusu uingie katika akaunti ukitumia tu alama ya kidole, uchanganuzi wa uso au kipengele cha kufunga skrini.
-
Rahisi
Funguo za siri huleta hali rahisi ambayo hutumia mbinu ya kufunga kifaa, kama vile alama ya kidole, uso, PIN au mchoro ili uingie katika Akaunti yako ya Google.
-
Salama
Funguo za siri hukupa ulinzi thabiti zaidi. Haziwezi kukisiwa wala kutumiwa upya, hali inayosaidia kuweka taarifa yako ya faragha kwa njia salama dhidi ya washambulizi.
-
Faragha
Data yako ya bayometriki, kama vile alama ya kidole au uchanganuzi wa uso, huhifadhiwa kwenye kifaa chako binafsi na haitawahi kushirikiwa na Google.
Rahisi sana
Ingia katika Akaunti yako ya Google, weka mipangilio ya ufunguo wako wa siri ukitumia kifaa chako na kila kitu kitakuwa tayari!