Drive logo

Gundua Vipengele vya Kuhifadhi kwenye Hifadhi ya Google

Mambo yako, utakavyo - Vipengele vya Hifadhi ya Google

 

Nafasi yako inafanya kazi na Hifadhi ya Google, Gmail na huduma ya Picha kwenye Google, kwa hivyo unaweza kuweka faili, kuhifadhi viambatisho vya barua pepe na kuweka nakala rudufu za picha kwenye Hifadhi ya Google kwa urahisi. Unaweza pia kununua nafasi ya ziada ya kuhifadhi kwenye wingu ukiihitaji.

Nembo ya nafasi isiyolipishwa ya GB 15 ya Hifadhi ya Google

Picha, video, mawasilisho, PDF - hata faili za Microsoft Office. Aina yoyote ya faili inaweza kuwekwa salama katika Hifadhi ya Google.

Aina ya faili zinazoweza kuwekwa katika Hifadhi ya Google ni pamoja na picha, hati na muziki

Faili zilizo katika Hifadhi ya Google huwa za faragha, hadi unapoamua kuzishiriki. Unaweza kuwaalika watu wengine, kwa urahisi, ili waangalie, watoe maoni na wabadilishe faili au folda yoyote unayochagua. Ni ushirikiano mtandaoni uliorahisishwa.

Chaguo za faragha na kushiriki za Hifadhi ya Google

Usalama wa faili zako ni jambo la umuhimu mkubwa. Ndiyo maana kila faili katika Hifadhi ya Google huwa salama licha ya kinachofanyika kwenye simu, kibao au kompyuta yako. Hifadhi ya Google imesimbwa kwa njia fiche ya SSL; itifaki ile ile ya usalama inayotumika kwenye Gmail na huduma zingine za Google.

Kufunga Hifadhi ya Google kwa ajili ya Usalama

Imeundwa kufanya kazi na Google

 
Kiambatisho cha picha kwenye Gmail kikihifadhiwa katika hifadhi kwa mbofyo mmoja

Fanya kiashiria kielee juu ya kiambatisho katika Gmail na utafute nembo ya Hifadhi ya Google. Hapo unaweza kuhifadhi kiambatisho chochote kwenye Hifadhi yako ili uweze kukipanga na kukishiriki kikiwa mahali pamoja na salama.

Kiambatisho cha picha kwenye Gmail kikihifadhiwa katika hifadhi kwa mbofyo mmoja

Hifadhi ya Google inaweza kutambua picha na maandishi yako katika hati zilizopigwa skani. Kwa hivyo unaweza kutafuta neno kama "Eiffel Tower" na upate hati za maandishi zilizo na maneno hayo na vilevile picha halisi za Mnara wa Eiffel.

Picha ya pwani ya Oregon iliyohifadhiwa kwenye Hifadhi ya Google na kushirikiwa kwenye Google+

Weka picha zako katika Hifadhi na uzione zikiwa maridadi katika huduma ya Picha kwenye Google. Pata, kwa urahisi, mwonekano uliohaririwa kitaalam, pamoja na uhuishaji, filamu na mengine mengi…

Data ya Hifadhi ya Google kwenye Chromebook

Hifadhi ya Google imejengewa ndani ya Chromebook, kwa hivyo faili na picha zako huhifadhiwa nakala rudufu kiotomatiki. Utapata GB 100 za hifadhi bila malipo kwa miaka miwili kwenye Chromebook nyingi mpya.

 

Fanya kazi kwa njia bora zaidi ukitumia programu

 

Unda hati na ushirikiane na watu wengine. Shiriki hati na faili, unda malahajedwali na uunde wasilisho ukiwa popote pale ukitumia Hati za Google, Majedwali ya Google na Slaidi za Google apps.

Hifadhi ya Google, Hati za Google, Majedwali ya Google na Slaidi za Google zinapatikana na zinaweza kushirikiwa

Fomu za Google hukuwezesha kufanya utafiti au kubuni orodha ya timu kwa haraka kwa kutumia fomu rahisi ya mtandaoni.

Mfano wa Fomu za Google kwenye Hifadhi ya Google

Weka picha na uunde chati za mtiririko kisha uziongeze kwenye hati zingine au uzibandike kwenye tovuti kwa urahisi ukitumia Michoro ya Google.

Aikoni ya Michoro ya Google

Hariri picha yako ya wasifu, rembesha mandhari, chora ramani ya mawazo yako na mengine mengi. Zaidi ya programu 100 za Hifadhi ya Google zinaweza kukusaidia kufanya mengi zaidi na hati zako. Zijaribu kwa kusakinisha moja kutoka kwenye Mkusanyiko wa Hifadhi ya Google katika Duka la Chrome kwenye Wavuti.

Zaidi ya programu 100 za Hifadhi ya Google zinapatikana

Tumia Hifadhi hata kwa mambo mengi zaidi

 
Mfano wa kuhifadhi hati kwenye Hifadhi ya Google kwa kupiga picha ukitumia simu ya Android

Piga skani ya hati zako zote za karatasi kwa kutumia Hifadhi ya Google kwenye Android, Hifadhi ya Google itaziweka papo hapo zikiwa katika muundo wa PDF.

Kubadilisha kati ya Hifadhi ya Google mtandaoni au nje ya mtandao

Fanya faili zipatikane nje ya mtandao ili uweze kuziona hata wakati simu au kompyuta yako kibao imepoteza huduma ya intaneti, kama kwenye ndege ama katika jumba ambalo lina muunganisho usio thabiti.

Mfano wa historia ya masahihisho ya faili ya Hifadhi ya Google

Unaweza kurejelea maelezo ya shughuli za hadi siku 30 zilizopita kwenye aina nyingi za faili, kwa hivyo ni rahisi kuona waliobadilisha chochote na urudi kwenye matoleo ya awali. Kufuatilia masasisho ya faili sasa kumerahisishwa.