Muhtasari wa vipengele
Zana za Kuingiza Data za Google zinaweza kukusaidia kucharaza kwa urahisi zaidi katika lugha unayoitaka. Kwa sasa tunatoa aina kadhaa za zana za kuingiza maandishi:
- IME (Programu Inayotambua Mbinu za Kuingiza Data) hufananisha micharazo yako ya vitufe na lugha nyingine ikitumia injini ya kubadilisha.
- Unukuzi wa mfumo wa kuandika hubadilisha sauti/fonetiki za maandishi katika lugha kwenda nyingine ambayo inalingana na sauti hiyo kwa karibu. Kwa mfano, unukuzi wa mfumo wa kuandika hubadilisha "Namaste" kuwa "नमस्ते" katika Kihindi.
- Kibodi pepe huonyesha kibodi kwenye skrini yako ambayo hufananisha vitufe na vilivyo kwenye kibodi yako ya kawaida. Unaweza kucharaza moja kwa moja katika lugha nyingine ukitumia mpangilio wa kibodi uliyo kwenye skrini.
- Kuandika kwa Mkono hukuruhusu kuchapa maandishi kwa kuchora herufi kwa vidole vyako. Kuandika kwa Mkono kwa sasa kunapatikana katika Kiendelezi cha Chrome cha Zana za Kuingiza Data za Google.
Pata maelezo ya jinsi ya kusanidi Zana za Kuingiza Data katika mipangilio ya Akaunti ya Google .
Pata maelezo ya jinsi ya kutumia Zana za Kuingiza Data katika bidhaa za Google, ikiwemo Gmail, Hifadhi, Tafuta na Google, Google Tafsiri, Chrome, na Mfumo wa Uendeshaji wa Chrome.
Ili kuijaribu, nenda tu kwenye ukurasa wetu wa majaribio.