Kiendelezi cha Mfumo wa Uendeshaji wa Chrome cha Zana za Kuingiza Data za Google
Kiendelezi cha Mfumo wa Uendeshaji wa Chrome cha Zana za Kuingiza Data za Google hukuruhusu kuandika katika lugha unayotaka kwenye Mfumo wa Uendeshaji wa Chrome.
Tofauti kuu kati ya kiendelezi hiki cha Mfumo wa Uendeshaji wa Chrome na kiendelezi cha Chrome cha Zana za Kuingiza Data za Google ni:
Kipengele | Kiendelezi cha Chrome | Kiendelezi cha Mfumo wa Uendeshaji wa Chrome |
---|---|---|
Mifumo ya uendeshaji inayoweza kutumiwa | Kivinjari cha Chrome kwenye kompyuta yoyote (Windows, Mac, Linux) | Kompyuta zenye Mfumo wa Uendeshaji wa Chrome pekee |
Je, inafanya kazi katika sehemu ya anwani (SanduKuu)? | La | Ndiyo |
Je, inafanya kazi nje ya mtandao? | La | Ndiyo |
Zana za Kuingiza Data zimewekwa pamoja na Chromebooks. Kama unatumia Chromebook iliyo na Toleo la 28 au zaidi, uko tayari kutumia Zana za Kuingiza Data. Vinginevyo, pata toleo jipya la Chromebook yako. Kama unatumia Mfumo wa uendeshaji wa Chromium, sakinisha kiendelezi cha Mfumo wa Uendeshaji wa Chrome kutoka kwa Duka la Wavuti wa Chrome.
Enda kwenye Mipangilio → Onyesha mipangilio mahiri → Lugha. Bofya kitufe cha "Lugha na mipangilio ya kuingiza data". Chagua zana ya kuingiza unayotaka kutumia. Kumbuka kwamba mbinu za kuingiza data zinazoitwa [Jina la lugha katika lugha ya asili] ([Jina la lugha katika Kiolesura cha lugha ya Chrome]), k.m., हिन्दी (Kihindi), kinaonyesha Zana za Kuingiza Data kwa unukuzi. Zana za unukuzi hubadilisha ingizo lako kifonetiki hadi lugha lengwa.
Baada ya kusanidi, washa mbinu ya kuingiza data unayotaka. Bofya mbinu ya kuingiza data inayotumika kwa sasa, kwa mfano, "Marekani" kwenye kizindua (yaani, upau/kidirisha cha arifa kilicho chini kwenye upande wa kulia wa skrini yako).
Orodha ya mbinu za kuingiza data zilizochaguliwa (ikiwa ni pamoja na zana za kuingiza data kutoka kwenye kiendelezi) zitaonekana. Chagua zana ya kuingiza data unayotaka kutumia. Ili kuongeza zana mpya ya kuingiza data, bofya "Badilisha lugha na uingizaji upendavyo...".
Kwa kuwa umechagua zana ya kuingiza data, sogeza kishale kwenye kisanduku chochote cha kuingiza (SanduKuu pia linaweza kutumiwa), unaweza kuanza kuacharaza.
Makala yanayohusiana kuhusu jinsi ya kutumia zana maalum za kuingiza data: