Unukuzi wa mfumo wa kuandika

Unukuzi wa mfumo wa kuandika unatumiwa na zaidi ya lugha 20. Angalia video zifuatazo ili upate maelezo zaidi kuhusu unukuzi wa mfumo wa kuandika na jinsi ya kuutumia. Pia jaribu kuutumia mtandaoni .

Unukuzi wa mfumo wa kuandika ni mbinu ya kubadilisha kutoka mfumo mmoja wa kuandika kwenda kwa mwingine kwa kuzingatia fonetiki zinazofanana. Ukiwa na zana hii, unacharaza katika herufi za Kilatini (k.m. a, b, c nk), ambazo hubadilishwa kuwa herufi ambazo zina matamshi sawa katika lugha lengwa. Kwa mfano, unukuzi wa mfumo wa kuandika kwa Kihindi, unaweza kucharaza "namaste" ili upate "नमस्ते", ambayo inatamkwa kama "Namaste". Unaweza kuonyeshwa orodha ya mapendekezo ya unukuzi wa mfumo wa kuandika tofauti ili uchague. Kumbuka kwamba "unukuzi wa mfumo wa kuandika " ni tofauti na "kutafsiri": ubadilishaji unazingatia matamshi, wala si maana.

Unukuzi wa mfumo wa kuandika hutumia ubadilishaji wa kifonetiki unaofanana kwa mbali. Unacharaza tu makisio yako bora ya matamshi katika herufi za Kilatini na unukuzi wa mfumo wa kuandika utayalinganisha na mapendekezo bora. Kwa mfano, "namaste" na "nemaste" zitabadilishwa kuwa "नमस्ते" kama pendekezo.

Kutumia unukuzi wa mfumo wa kuandika, hatua ya kwanza ni kuwasha Zana za Kuingiza Data. Fuata maelekezo ili uwashe Zana za Kuingiza Data katika Huduma ya Tafuta na Google, Gmail, Hifadhi ya Google, Youtube, Google Tafsiri, Chrome na Mfumo wa Uendeshaji wa Chrome.

Unukuzi wa mfumo wa kuandika unawakilishwa na herufi kutoka lugha lengwa, kama vile . Kubofya ikoni ili kuwasha/kuzima unukuzi wa mfumo wa kuandika wa sasa au kubofya kishale kilichokaribu nao ili uchague zana nyingine ya kuingiza data.Unukuzi wa mfumo wa kuandika unapowashwa, kitufe huwa kijani iliyokolea .

Unapotumia unukuzi wa mfumo wa kuandika, charaza neno kifonetiki ukitumia herufi za Kilatini. Unapocharaza, utaona orodha ya maneno yanayopendekezwa ambayo yanafanana na tahajia ya fonetiki. Unaweza kuchagua neno kutoka kwenye orodha kwa kufanya lolote kati ya yafuatayo:

  • Bofya "SPACE" au "ENTER" ili uchague pendekezo la kwanza,
  • Bofya neno lenyewe,
  • Ingiza nambari iliyo kando ya neno,
  • Kagua orodha ya mapendekezo katika ukurasa kwa vitufe vya vishale vya "UP"/"DOWN". Pindua kurasa ukitumia vitufe vya "PAGEUP"/"PAGEDOWN". Bonyeza "SPACE" au "ENTER" ili uchague neno lililoangaziwa