Hifadhi/Hati za Google

Angalia video hapo chini ili upate maelezo ya haraka ya jinsi ya kuwasha Zana za Kuingiza Data katika Hifadhi ya Google/Hati za Google.

Kuna njia tatu za kuwasha Zana za Kuingiza Data katika Hifadhi ya Google:

  1. Badilisha mipangilio ya lugha ya mtumiaji iwe lugha ambayo ungependa kucharaza. Ili kufanya hivi, fuata maelekezo haya.
  2. Badilisha mipangilio ya lugha ya hati iwe lugha ambayo ungependa kucharaza. Ili kufanya hivyo, unda hati mpya au ufungue hati iliyopo. Nenda kwenye Faili → Lugha. Kisha, uchague lugha ambayo ungependa kutumia.
  3. Washa Zana za Kuingiza Data katika Gmail.

Zana za Kuingiza Data zinapowashwa, utaona ikoni upande wa kulia (au upande wa kushoto juu ya ukurasa wa RTL) wa upau wa vidhibiti.

Makala yanayohusiana kuhusu jinsi ya kutumia zana maalum za kuingiza data:

Machapisho ya blogu za Google yanayohusiana: