Kibodi Pepe
Kibodi pepe, au kibodi "ya skrini", hukuruhusu kucharaza moja kwa moja ukitumia hati ya lugha yako asili kwa njia rahisi na dhabiti, bila kujali ulipo au kompyuta unayotumia. Baadhi ya matumizi ya kawaida ya kibodi pepe ni pamoja na:
- Kumruhusu mtu kucharaza katika lugha yake mwenyewe kwenye kibodi za kigeni - kama vile anaposafiri nje ya nchi au wakati anaishi katika nchi nyingine,
- Kuwezesha hali nzuri zaidi ya kucharaza kwa kuruhusu kucharaza kupitia kubofya kwenye skrini,
- Kutoa njia ya haraka na rahisi ya kubadilisha kati ya misimbo ya herufi tofauti na/au alfabeti.
Kibodi pepe hutumika katika zaidi ya kibodi 100 kwa zaidi ya lugha 70. Angalia video hii ya mafunzo ili upate maelezo ya jinsi ya kutumia kibodi pepe. Pia ijaribu mtandaoni.
Ili kutumia kibodi pepe, hatua ya kwanza ni kuwasha Zana za Kuingiza Data. Fuata maelekezo ili uwashe Zana za Kuingiza Data katika Huduma ya Tafuta na Google, Gmail, Hifadhi ya Google, Youtube, Google Tafsiri, Chrome na Mfumo wa Uendeshaji wa Chrome.
Kibodi pepe huwakilishwa na ikoni ya kibodi . Bofya ikoni ili kuwasha/kuzima Mbinu
za kuingiza data za sasa au bofya kishale kilichokaribu nayo ili uchague zana nyingine ya
kuingiza data. Kibodi pepe inapoanza kutumiwa, kitufe hubadilika na kuwa rangi ya kijivu
iliyokolea
.
Tumia kibodi pepe kwa kucharaza kwenye kibodi yako mwenyewe kana kwamba ni kibodi pepe, au kwa kubofya vitufe kwenye kibodi pepe moja kwa moja ukitumia kipanya chako.
Ili kupunguza kibodi kilicho kwenye skrini, bofya kishale kilicho sehemu ya juu kulia ya kibodi iliyo kwenye skrini.