Kuandika kwa mkono
Kuingiza data kwa kuandika kwa mkono hukuruhusu kuandika maneno moja kwa moja ukitumia kipanya ama padi. Kuandika kwa Mkono kunatumika kwa zaidi ya lugha 50.
Ili utumie kuingiza kwa kuandika kwa mkono, hatua ya kwanza ni kuwasha Zana za Kuingiza Data. Fuata maelekezo ili uwashe Zana za Kuingiza Data katika Huduma ya Tafuta na Google, Gmail, Hifadhi ya Google, Youtube, Google Tafsiri, Chrome na Mfumo wa Uendeshaji wa Chrome. Kumbuka kwamba kuingiza kwa kuandika kwa mkono kwa baadhi ya lugha huenda hakupatikani katika baadhi ya bidhaa zilizopo hapo juu.
Tazama video hii ya mafunzo ili upate maelezo ya jinsi ya kutumia kuingiza data kupitia kuandika kwa mkono katika kiendelezi cha Chrome cha Zana za Kuingiza Data za Google.
Kuingiza data kwa kuandika kwa mkono kunawakilishwa na ikoni ya kalamu .Wakati wa kutumia kuingiza
data kwa kuandika kwa mkono, sogeza padi/kipanya chako hadi kwenye paneli ya kuandika kwa
mkono. Endelea kubonyeza padi/kipanya ili uchore herufi. Herufi zinazopendekezwa
zinazofananisha mwandiko wa mkono wako zitaonekana. Chagua pendekezo kwa kubofya herufi,
au ubonyeze kitufe cha "ENTER" au "SPACE" ili uchague pendekezo la
kwanza.